THE FACE

Saturday, August 18, 2012

NYWELE




NYWELE zinatakiwa kutunzwa vizuri na kulindwa ili zisiharibike kwa njia yoyote.  Ukiosha nywele zako na baadaye kutumia shanuo ama brashi kuzibana, unaweza kuzifanya zikatike, au hata kuathiri ukuaji wake.

 Fuata hizi dondoo rahisi ambazo ili kuzifanya nywele zako zikue vizuri na kupendeza.

Wanaotumia  jell,
Kama unatumia jelly ya nywele katika mtindo wako, hakikisha unaosha vizuri nywele zako na kuondoa jeli yote kabla ya kwenda kulala.

Unapolala na jelly au urembo mwingine unasababisha kuziba kwa tundu za nywele katika ngozi ya kichwa. Kitendo hicho mbali na kuzuia kupumua kwa ngozi ya kichwa, huchangia kuzuia nywele chipukizi kuota katika ngozi ya kichwa.

Kuwa makini na shampoo za dukani
Mara nyingi baadhi ya watengenezaji wa vipodozi huweka maslahi mbele bila kuangalia athari zinazoweza kuwapata watumiaji wa bidhaa zao.

Kuna baadhi ya shampoo huwa na kemikali hatari kwa ngozi. Hivyo ni vizuri zaidi kama utakuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na aina hiyo ya kipodozi.

Pendelea zaidi kutumia herbal shampoo. Si hivyo tu, wakati mwingine vipodozi vya bei rahisi huwa na kasoro, hivyo ni vyema kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa nywele kujua aina gani ya shampoo ni sahihi kwa nywele zako.
Kinyume cha hapo unaweza kuishia kuathiri nywele na ngozi yako bila kufahamu.

Epuka kubana nywele mara kwa mara
Ubanaji wa nywele hasa kuelekea mgongoni mara nyingi huhatarisha maisha ya nywele hasa za usoni. Nywele maana yake lazima zivutwe hasa zilizombali na unapozinania hivyo zinazeza kukatika hasa zilizo hafifu. Nywelie za sehemu ya usoni ndiyo huathirika zaidi.

Usichane nywele zikiwa mbichi
Zinapokuwa mbichi nywele huwa na uwezekano mkubwa wa kukatika hasa zinapochanwa au kufutwa kwa tautlo gumu. Ni vyema ukaacha zikauke kwa upepo ndipo uzichane.

Kama utakuwa unatumia ‘conditioner’ hakikisha husugui katika nywele, badala yake tumia kwa kupaka. Kama nywele zako zimekatika na hazilingani, ni vyema ukakata ncha ili kuzisawazisha. Hii husaidia kuzifanya zikue vizuri na pia kuondoa uwezekano wa kukatika zinapoingia maji. Hasa kwa zile zenye ‘relaxer’.

Chochea ukuaji wa nywele kwa kuzichana
Unapochana nywele zako hakikisha unatumia shanuo la mbao au kitana chenye meno yaliyoachana. Hakikisha nywele zako zinakuwa kavu. Usizivute sana kwani licha ya kusabaisha maumivu pia huleta uwezekano wa kukatika.

Nywele zinapochanwa husaidia  kuchochea mzunguko wa damu katika ngozi ya kichwa na kukua kwake.

No comments:

Post a Comment