THE FACE

Sunday, September 2, 2012

rangi katika Mitindo

 





Wanawake wengi wamekuwa wakipendelea kuvaa mavazi yenye rangi zinazowafanya waonekane wambamba zaidi ya maumbo yao, kwani baadhi yao huvaa tu nguo kiholela bila kuelewa rangi hizo zinamaana gani.
Na wakati mwingine rangi uipendayo inaweza isiwe rangi mahususi katika mavazi yako na ukitaka kwenda na wakati yakupasa kuchagua mavazi yenye taswira na muonekano wako na pia yatakayokufanya ujisikie vizuri kwneye uvaaji wako.
Ni rangi zipi zenye kufanana na je! rangi zinamaanisha nini? Embu tutazame baadhi ya rangi kwenye mavazi yako ya kila siku:
Nyeusi: Rangi hii huwa na matumzi mengi kwani itakufanya uonekane mwembamba kuliko umbo lako halisi na mwenye kujiamini.
Pinki: Kwa kawaida rangi hii huwa ni ya kike zaidi na humfanya mvaaji kuonekana mcheshina wakati mwingine huonekana huwa na umri mdogo tofauti na umri wake halisi. Kwani wabunifu wengi huifafanua kwamba rangi hii ni kama rangi ya kitoto hasa kwa zile tamaduni za Ughaibuni.
Nyekundu: Mavazi yanayotokana na rangi hii huelezea umakini na uthubutu ambao huonekana kwa mvaaji tu.
Bluu: Rangi hii huvutia zaidi kwa wanawake wanaojitegemea, ambao mara nyingi hujisikia raha zaidi kuwa pekee na wenye kufurahia mafanikio yao.
Rangi ya Machingwa: Hii humaanisha kuwa unapenda kuonekana miongoni mwa watu wengi, mwenye kufurahia changamoto na mwenye tabia ya kuonekana upo juu.
Njano: Hii ni rangi yenye kuonekana zaidi, mavazi ya rangi hii huashiria kujiamini zaidi na kuelezea kwa urahisi muonekano wa mvaaji.
Nyeupe: Na rangii hii huashiria amani na usalama. Wale wanaochagua mavazi ya rangi hii huchagua usalama na pia ni rangi yenye kuoana na rangi zote. Mbali na hilo pia hukufanya uwe mpana zaidi pia hukubalika kuwa ni rangi yenye upendo zaidi ya nyingine.
Kijani: Hii ni rangi inayoashiria uoto wa asili, hivyo mavazi ya rangi kama hii humaanisha huvaliwa sana sana na watoto.
Kwa kuwa kila mmoja wetu huvaa rangi anayoipenda ya mavazi ni vizuri kuwa makini nazo katika kuoanisha rangi ya ngozi yako na rangi ya vazi uvaalo, ili kupata matokeo mazuri.
Na sivizuri kuiga rangi za Utamaduni wa watu wengine, bila kujua athari zake katika mitindo.
Pia Rangi kama za Kijani, Njano na Nyekundu ndizo rangi sahihi huvaliwa na watoto wa Kiafrika. Yakupasa kulizingatia hilo katika kuchagua mavazi ya watoto.
Na rangi kama ya Pinki na Nyeupe nazo siyo rangi sahihi kwa watoto wa Kiafrika.

No comments:

Post a Comment