THE FACE

Saturday, August 18, 2012

KOKOLIKO DESIGNS


KOKOLIKO DESIGNS BY AISHA KISOKI


WADAU HUYU NI DADA AISHA KISOKI AKA MAMA WA SOFIA PRODUCTION AMBAYE ANASHUGHULIKA NA UCHUKUAJI WA VIDEO (VIDEO PRODUCTION) NA VILEVILE NI MBUNIFU WA MITINDO YA NGUO KWA KUTUMIA RASILIMALI ZA KITANZANIA KAMA BATIKI.VITENGE,NA MATERIALS NYENGINE.
NILIPATA BAHATI YA KUBADILISHANA NAE MAWAZO KUHUSU FANI NZIMA YA  MITINDO NA KUNIAHIDI KAMA ATAFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KWENYE FANI HII YA MITINDO  KWA KUTOA HAMASA KWA WATANZANIA KUTUMIA NGUO ZILIZOTENGENEZWA NA VITAMBAA VYETU.
ANABUNI KWA KUTUMIA MATERIALS YOTE YA KITANZANIA KAMA BATIKI,KIKOI,MASAI.PIA ALINIONYESHA BAADHI YA KAZI ZAKE AMBAZO TAYARI ZIKO NDANI YA STOCK KWA AJILI YA KUJIPANGA NA ONYESHO .
Mama Sofia Production akiwa kwenye pozz huku amevalia moja kati ya mavazi anayobuni yeye mwenyewe. Pamoja na maswala ya Video na Audio....mama huyu pia ana kampuni ya mavazi inayojulikana kama KOKOLIKO MODEL yenye maskani yake hapa jijini Tanga.

Miongoni mwa wanamitindo wanaovaa nguo za kampuni hiyo.

Hapa akionyesha baadhi ya nguo ambavo zinapatikana ofisini kwake.

Mavazi Ya Kiafrika
KWA TAARIFA ZAIDI ZA MITINDO YAKE NA ONYESHO ANALOKUSUDIA KULIFANYA  NITAWAPA TAARIFA BAADAYE MARA BAADA YA KUKAMILISHA MCHAKATO  MZIMA. KWA WALE AMBAO WATAPENDA KAZI ZAKE NA KUTAKA KUNUNUA NITAWAPA CONTACT ZAKE. ILA KWA SASA ANAPATA TANGA INDIA STREET KARIBU NA ECKERNFORDE SECONDARY AU TEXAS PUB NDANI YA OFISI YA SOFIA PRODUCTION.

1 comment:

  1. Habari! mnapatikana wapi au bidhaa zenu zinapatikana maeneo yapi na yapi kwa usambazaji?

    ReplyDelete